1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius yupo Ukraine

21 Novemba 2023

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amewasili hii leo nchini Ukraine ili kuthibitisha tena uungaji mkono wa Berlin kwa Kyiv katika mapambano yake dhidi ya wanajeshi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4ZFaK
Ukraine Kiew | Boris Pistorius, deutscher Verteidigungsminister
Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Ni ziara ya pili ya Pistorius mjini Kyiv na inajiri siku moja baada ya ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.Kyiv imekuwa na wasiwasi kuwa vita vya Mashariki ya kati vingesababisha kupungua kwa msaada kutoka kwa washirika wake. Ujerumani ambayo ni mfadhili mkuu wa pili wa msaada wa kijeshi kwa Ukraine baada ya Marekani, inalenga kuondoa hofu hiyo ya Ukraine.Pistorius anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati huu Urusi ikizidisha mashambulizi yake nchini humo. Watu watatu wameuawa kufutia mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo katika mikoa ya mashariki mwa Ukraine ya Kharkiv na Donetsk.