SiasaGeorgia
Georgia yaachana na sheria yenye utata
10 Machi 2023Matangazo
Muswada huo ulipigiwa kura wa kuondolewa baada ya kusomwa kwa mara ya pili, baada ya mbunge mmoja kati ya wabunge 36 waliopiga kura kuunga mkono sheria hiyo ambayo wakosoaji wanailinganisha na sheria za Urusi ambapo mamlaka imekuwa ikiwanyamazisha wapinzani wa Ikulu ya Urusi, Kremlin.
Mamia ya waandamanaji wanaoipinda serikali walikusanyika nje ya majengo ya bunge wakati kura hiyo inapigwa. Viongozi wa Georgia wamekosolewa vikali kimataifa kutokana na kudhoofika kwa demokrasia na kuharibu uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.