1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Visa vya ukiukaji wa haki za binadamu vyaendelea Sudan

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMy

Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la umoja wa mataifa imesema kwamba vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu bado vinaendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Wachunguzi wa shirika hilo wanaofuatilia hali ya haki za binadamu katika jimbo la Darfur wamesema ijapo kuwa serikali ya Sudan inatekeleza hatua za kurekebisha hali hiyo lakini hatua zenyewe zinakwenda pole pole mno.

Ripoti hiyo ya kwanza imewasilishwa tangu mapendekezo kadhaa yalipofikishwa katika serikali ya mjini Khartoum mwezi Juni.

Baadhi ya mapendekezo hayo yalihusu kuchunguza mashambulio dhidi ya raia na visa vya kuwaajiri watoto kwenye vikosi vya askari.