1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Myanmar yakosolewa na ILO kuhusu mifumo yake ya kazi

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1O

Myanmar imekosolewa vikali na Shirika la Kazi Ulimwenguni ILO kwa kuendeleza mifumo ya kazi ya lazima.Katika kikao maalum cha Shirika hilo hali ya wafanyikazi nchini Myanmar ilifanyiwa tathmini na kuamua kuahirisha kuichukulia hatua ya ya kimataifa ya kisheria.Myanmar iliridhia kujaribu kutafuta suluhu kwa waathiriwa ndipo shirika hilo likaamua kuchukua hatua hiyo.Kwa mujibu wa taarifa ya sekretariat ya shirika la ILO mpango huo huenda usifue dafu kwani wengi ya wafanyikazi hawatahusishwa.Balozi wa Myanmar katika shirika hilo la wafanyikazi anasisitiza kuwa hakuna anayeruhusiwa kukiuka sheria za kazi nchini mwake.Serikali ya uongozi wa kijeshi wa Myanmar umepiga marufuku kazi ya kulazimishwa ila kulingana na makundi ya kutetea haki za binadamu hakuna hatua zozote zinazochukuliwa hususan kwenye maeneo ambayo hayatembelewi na watalii.

Kwa upande mwingine wanaharakati wengine watatu wanaopinga serikali wamekamatwa huku mchunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Paulo Sergio Pinheiro aliyeko nchini humo akisistiza kuwa hatua hiyo imesitishwa.Watu hao walikamatwa walipokuwa wakisambaza vikaratasi vinavyokosoa serikali katika soko la Mingalar mjini Yangon.