GENEVA: Maafikiano kuhusu ukaguzi wa hali ya haki za binadamu
19 Juni 2007Matangazo
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limekubaliana na sheria zitakazowataka wanachama wa Baraza la Usalama,ikiwa ni pamoja na China, kuruhusu ukaguzi wa mara kwa mara kuhusu rekodi zao za haki za binadamu.Baraza hilo linasema,hali ya haki za binadamu ni mbaya,hasa nchini Korea ya Kaskazini,Cambodia na Sudan.Wakati huo huo Cuba na Belarus zimeondoshwa kutoka orodha ya nchi zilizolaumiwa kukiuka haki za binadamu. Baraza la Haki za Binadamu,liliundwa mwaka jana. Lakini baadhi ya wanachama wa Umoja wa Mataifa wanasema baraza hilo halina usemi mkubwa.