1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Kiwanda cha kinuklia cha Iran kimeanza kufanya kazi upya

9 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmf

Shirika la Nishati ya kinuklia la Umoja wa Mataifa linatazamia kuwa na mkutano wa dharura leo jumanne,kulijadili suala la Iran kuanzisha tena kazi kwenye kinu cha kinuklia cha Isfahan.Iran ilianzisha upya utaratibu wa kusafisha yuranium,licha ya kuonywa na wapatanishi wa Umoja wa Ulaya kuwa suala hilo huenda likafikishwa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kwa uwezekano wa kuweka vikwazo dhidi ya Tehran.Katika jeribio la kutaka kuisadikisha Iran iachilie mbali mradi wake wa kinuklia unaoweza kutumiwa kutengeneza mabomu, Umoja wa Ulaya ulipendekeza kuipa Iran vichocheo vya kibiashara na kisiasa.Iran lakini imeukataa mpango huo na imesema mapendekezo ya Umoja wa Ulaya hayawezi kukubaliwa kwani Iran inanyimwa haki ya kujitengenezea nishati ya kinuklia.