GENEVA: Israel ilivunja haki za binaadamu katika vita vya Lebanon
22 Novemba 2006Wachunguzi wa haki za binaadamu wa Umoja wa mataifa wamesema mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon mwaka huu, yalikuwa ni adhabu bila kujali na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa kuhusu maswala ya kibinaadamu. Wataalamu watatu waliotumwa nchini Lebanon na Umoja wa mataifa kuchunguza juu ya vita vya Israel vya hivi karibuni dhidi ya Hezebollah nchini Lebanon, wamesema katika ripoti yao kwamba Israel ilishambulia bila hata kuwatahadharisha raia juu ya mashambulizi yake na kwamba ilitumia kupita kiasi mabomu ya mtawanyiko.
Nchi za magharibi zimesema uchunguzi huo ulifanyika katika upande moja na hukuzingatia mashambulizi ya makombora ya Hezbollah kwenye miji nchini Israel.
Kiasi cha raia wa Lebanon 1000 waliuawa katika vita hivyo vilivyodumu wiki nne.