Gebresselasie kustaafu mashindano ya riadha
12 Mei 2015Meneja wa mwanariadha huyo kutoka Ethiopia mwanzoni amesema Gebreselassie hajafika mwisho wa muda wake wa kukimbia , lakini baadaye alitoa taarifa kwa waandishi habari akisema mkimbiaji huyo amestaafu michezo ya riadha.
Gebreselassie amenukuliwa akisema kwamba "Nastaafu katika mbio za mashindano na sio kukimbia. Huwezi kuacha kukimbia , haya ndio maisha yangu. Bado nafurahia ziara yangu ya kuaga kama leo mjini Manchester."
"Kwangu mimi , sitaki kuacha kukimbia . Nataka kukimbia hadi kufa. Ndio huu ndio mpango wangu."
Gebreselassie anataka sasa kujishughulisha zaidi na shughuli za biashara na miradi ya ujenzi wa nyumba, anamiliki hoteli nne, shamba la kahawa na huuza magari.
Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae / ape / afpe
Mhariri: Iddi Ssessanga