GAZA.Viongozi wa ´Hamas na Fatah kukutana Mecca
5 Februari 2007Matangazo
Makubaliano ya kusimamisha mapigano baina ya wafuasi wa Hamas na Fatah yameonyesha dalili ya kutekelezwa baada ya watu zaidi ya 20 kuuwawa kufuatia mapambano baina ya pande hizo mbili yaliyozuka mapema alhamisi iliyopita.
Habari zaidi zinafahamisha kuwa wapiganaji wa pande zote mbili wameanza kuondoka katika mitaa ya Ukanda wa Gaza na maduka mengi yamefunguliwa tena.
Akizungumza mjini Damascus, Syria kiongozi wa hamas Khaled Meshaal ametoa mwito kwa wafuasi wa vyama hivyo kuacha mapigano kwa manufaa ya wapalestina wote.
Bwana Meshaal na waziri mkuu wa palestina Ismail Haniya wanatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas katrika mji wa Mecca nchini Saudi Arabia hapo kesho.