GAZA:Mkuu wa Shirika la Ujasusi wa Misri akutana na wanamgambo wa Kipalestina.
30 Agosti 2005Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Misri,Omar Suleiman amefanya mazungumzo tofauti na viongozi wa makundi ya wanamgambo wa Kipalestina,akiwa katika jitahada za mwisho kuwapooza waache munkari,kabla Israel haijakamilisha operesheni yake ya kuondoka maeneo ya Ukanda wa Gaza,itakayomaliza miongo minne ya kukalia ardhi za Wapalestina.
Bwana Seleiman amefanya mazungumzo na viongozi wa Fatah,Hamas na Islamic Jihad na baadae atalihutubia Bunge la Palestina kwa niaba ya Rais wa Misri Hosni Mubarak.
Kesho mkuu huyo wa idara ya ujasusi ya Misri atakwenda Jesusalem kwa mazungumzo na viongozi wa Israel,yatakayolenga juu ya maandalizi ya namna watakavyosimamia uvukaji wa watu na bidhaa katika mpaka wa Gaza na Misri,jukumu ambalo Wapalestina wanasisitiza Israel waliache wakati itakapokuwa inakabidhi udhibiti wa Gaza kwa Mamlaka ya Wapalestina katika siku chache zijazo.