GAZA:Hamas yasema iko tayari kuzungumza na Fatah
11 Oktoba 2007Kiongozi wa kundi la Hamas ambae pia ni waziri mkuu wa zamani wa Palestina Ismail haniya amesema chama chake kitafanya mzungumzo ya maelewano na chama cha Fatah kinacho ongozwa na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Bwana haniya ameeleza kwamba utawala wa Hamas mjini Gaza ni muda mfupi tu.
Serikai ya umoja wa kitaifa iliyoundwa na bwana Ismail Haniya ilifutwa kazi na rais Abbas baada ya kuutwaa Ukanda wa Gaza.
Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema hakuna mazungumzo yoyote yatakayofanyika na chama cha Hamas mpaka chama hicho kitakapoacha kuudhibiti Ukanda wa Gaza na kuutambua utawala wake.
Wakati huo huo rais Mahmoud Abbas amessisitiza kuwa taifa huru la Palestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza lazima liwe na ukubwa sawa na wakati majeshi ya Israel yalipoliteka eneo hilo katika vita vya mwaka 1967.
Hii ni mara ya kwanza kiongozi huyo ametamka wazi juu ya mipaka ya taifa hilo ambayo inapaswa kuzingatiwa katika makubaliano ya amani na Israel.
Matamshi hayo ya rais Abbas ameyatoa kabla ya mkutano unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao utakao jadili taifa huru la Palestina unaodhaminiwa na Marekani.