GAZA.Hamas na Fatah karibu kufikia makubaliano juu ya kumchagua waziri mkuu mpya
13 Novemba 2006Chama kinachotawala cha Hamas na chama cha Fatah cha rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas vimesema kuwa viko karibu kufikia makubaliano ya kumchagua waziri mkuu mpya atakae iongoza serikali ya umoja wa kitaifa.
Mohammad Shabir mkuu wa zamani wa chuo kikuu cha kiislamu mjini Gaza anatarajiwa kuchukuwa wadhfa huo kutoka kwa waziri mkuu wa sasa Ismail Haniyah.
Hata hivyo uwamuzi wa mwisho utafanywa na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Pande hizo mbili zinatarajia hatua ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa italegeza msimamo mkali wa Marekani na nchi za umoja wa ulaya na hatimaye nchi hizo kufungulia tena misaada kwa nchi ya Palestina.
Nchi za magharibi ziliweka vikwazo dhidi ya utawala wa Hamas mara tu chama hicho kiliponyakuwa ushindi dhidi ya chama cha Fatah katika uchaguzi wa mwezi Januari.
Marekani na nchi za umoja wa ulaya zinaitaka Palestina iitambue Israel pamoja kulaani vitendo vya ghasia.