1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Gaza mapigano yazidi baina ya Hamas na Fatah

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs6

Mapigano yanaendelea kuzagaa ndani ya mamlaka ya wapalestina kati ya makundi hasimu ya Fatah na Hamas .

Kiasi cha watu 47 wameuwawa kwenye mapigano hayo yaliyoanza siku ya jumamosi katika ukanda wa Gaza.

Waziri wa habari katika mamlaka ya wapalestina Mustafa Barghouti hapo jana ameutolea mwito Umoja wa ulaya kuisadia Palestinakabla mambo hayajaharibika zaidi.

Hapo jana wanachama wa Hamas waliokuwa na silaha walivamia kambi ya upande wa Fatah katika Gaza.Chama cha Hamas kinasema kimedhibiti kambi kadhaa za vikosi vya usalama kufuatia mapigano hayo.

Mawaziri kutoka upande wa chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas wamejiondoa kwa muda kwenye serikali ya umoja wa kitaifa na Hamas hadi pale mapigano yatakapokomeshwa.

Kiongozi wa Fatah rais Mahmoud Abbas amewashutumu viongozi wa Hamas kwa kupanga njama ya kufanya mapinduzi ya kijeshi. Umoja wa Ulaya tayari umezungumzia wasiwasi wake juu ya hali hiyo na kuonya juu ya uwezekano wa kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.