1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Viongozi wa Fatah na Hamas wakutana.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0q

Maafisa wa vyama vya Fatah na Hamas nchini Palestina wamekutana katika ukanda wa Gaza kwa lengo la kupambana na hali ya ghasia inayoendelea baina ya vyama hivyo viwili hasimu.

Huu ni mkutano wa kwanza wa maafisa wa ngazi ya juu katika muda wa wiki kadha.

Mvutano wa kuwania madaraka baina ya Hamas na Fatah ulizusha mapigano mwezi huu kati ya watu wenye silaha ambapo kiasi watu 19 wameuwawa.

Wiki kadha za mazungumzo kati ya chama cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas cha Fatah na kile cha Hamas juu ya kujaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa , na pengine kumaliza ghasia hizo , hadi sasa zimeshindwa.