1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY:Hakuna makubaliano bado kati ya Hamas na Fatah juu ya serikali ya umoja wa kitaifa

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvG

Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu Ismail Haniyeh wameshindwa kuafikiana juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Viongozi hao wawili wa palestina walikutana hapo jana kwa zaidi ya saambili huko Gaza kukiwa na ripoti kwamba pande hizo mbili huenda zikakubaliana juu ya suala hilo lakini kwa mujibu wa maofisa mazungumzo hayo yaliambulia patupu.

Hata hivyo viongozi hao wanatazamiwa kukutana tena leo kujaribu kuondoa tofauti zao zinazozuia kuundwa kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Awali hapo janamaofisa wa kundi la Hamas walifahamisha kuwa wameshafikia makuliano na chama cha Fatah kimsingi kuunda serikali mpya lakini hakueleza iwapo walikubaliana na matakwa ya Abbas kwamba kundi hilo la Hamas likubaliane na mikataba ya mpito ya awali na serikali ya Israel na kutambua haki ya kuwepo kwa taifa hilo.