1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY : Mapambano kati ya Fatah na Hamas yaendelea

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVG

Hakuna dalili ya kumalizika kwa umwagaji damu kati ya makundi hasimu ya Kipalestina ya Fatah na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Mapambano kati ya makundi hayo yamekuwa yakiendelea licha makubaliano ya kusitisha mapigano ya hivi karibuni yaliofikiwa na pande hizo mbili ambayo yalikuwa yaanze kufanya kazi hapo Ijumaa.Muhanga wa hivi karibuni inarepotiwa kuwa ni afisa usalama wa Fatah ambaye ameuawawa kwa kupigwa risasi karibu na makao makuu ya chama hicho mjini Gaza.

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ambaye ni wa chama cha Fatah na kiongozi wa Hamas Khaled Meshall wamekubali kukutana katika mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia hapo Jumanne kujaribu kutafuta suluhisho la kukomesha mapigano.