1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gauck ataka siasa itumikie nchi

20 Machi 2012

Baraza la Shirikisho la Ujerumani limemchagua Joachim Gauck kuwa rais mpya wa Ujerumani kuchukuwa nafasi ya Christian Wulff aliyelazimika kujizulu kwa kile kilichoitwa kuivunjia heshima taasisi ya uraisi.

https://p.dw.com/p/14Mce
Berlin/ Bundespraesident Joachim Gauck (M.) laechelt am Sonntag (18.03.12) in Berlin waehrend der Bundesversammlung im Reichstag nach seiner Wahl. Mit ueberwaeltigender Mehrheit ist der fruehere Leiter der Stasi-Unterlagenbehoerde im ersten Wahlgang von den Delegierten der Bundesversammlung in das hoechste Staatsamt der Bundesrepublik Deutschland gewaehlt worden. (zu dapd-Text) Foto: Axel Schmidt/dapd
Bundespräsidentenwahl 2012 Bundespräsident Joachim GauckPicha: dapd

Je, huyu ni rais aliyezivuna nyoyo za watu? Ndilo suali linalojibika kwa kuangalia kiwango cha kukubalika kwa Joachim Gauck. Vyama vyote vinavyounda serikali pamoja na upinzani, ukiacha chama cha Die Linke, vimemuunga mkono mwanaharakati huyu wa zamani wa haki za binaadamu chini ya utawala wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kuwa raisi mpya wa Shirikisho la  Jamhuri ya Ujerumani.

Ana asilimia 80 wa Wajerumani wanaomuunga mkono. Hapana shaka, huu ni mguu mzuri kwa Gauck kupandia jukwaani. Sababu ni kuwa anataka awe rais wa watu, ambaye anapigania kuwapo midahalo. Mada ya midahalo hiyo haikwepeki, nayo ni juu ya namna ambavyo watu wangependa kuongozwa. Ni mtu anayetaka siasa na wanasiasa waihudumie nchi.

Siasa inamtegemea Gauck kuirudishia taasisi ya urais heshima yake, ambayo imepokwa na mtangulizi wake, Christian Wullf. Umma unamtaka ajikite zaidi katka masuala ya haki za kijamii, sera bora zaidi za familia, na maingiliano zaidi ya Ujerumani miaka 22 baada ya kuungana tena kwa Mashariki na Magharibi.

Mambo haya ndiyo yaliyomkalia karibu Gauck, na sio mgogoro wa fedha katika kanda euro wala siasa za nje za Ujerumani. Kwake ni kuzileta pamoja siasa na jamii, akiamini kuwa ni pale tu hivyo vinapoletwa katika mfumo utawala, ndipo panapopatikana fursa ya kuwapo kwa demokrasia ya kweli, haki na uhuru binafsi.

Der neue Bundespräsident Joachim Gauck (2.v.l) bekommt am Sonntag (18.03.2012) Blumen von Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) nach seiner Wahl durch die Bundesversammlung im Reichstag in Berlin. 1240 Wahlleute bestimmten den neuen Bundespräsidenten. Foto: Kay Nietfeld dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Bundespräsidentenwahl 2012 Bundespräsident Joachim GauckPicha: picture-alliance/dpa

Uwajibikaji na uhuru ni mambo mawili ya thamani ambayo Gauck anajinasibisha nayo, akiwa na sababu nzuri na akiwa na uzoefu wa kutosha. Alizaliwa kwenye Ujerumani ya Mashariki iliyo chini ya utawala usioheshimu haki za kiraia hapo mwaka 1940, naye akapambana na utawala huo kuzipigania haki hizo.

Hivi leo, katika Ujerumani ya kidemokrasia, anasisitiza kwamba raia wanatakiwa wazipate haki hizo kwa ukamilifu, anataka pawepo na midahalo ya kuzisawasisha siasa. Gauck anazipinga sana siasa za kutojali, akiziona kama utamaduni mbaya wa kutokuridhika kwa Ujerumani. Anaona ni muhimu kwa watu wenyewe kujihushughulisha kwa kiwango kikubwa na siasa za nchi, ili kwavyo maendeleo na mafanikio yapatikane.

Na hii isifahamike vibaya: hayo si mambo ambayo Gauck anayaamini kwa sababu ya kushika ofisi ya uraisi tu. Bali hayo yamekuwa ndiyo maudhui ya maisha yake, utamaduni wake na nguvu yake. Akiwa mchungaji katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Gauck alikuwa sehemu ya vuguvugu la "Wir sind das Volk! - sisi ndio umma wenyewe - lililokuwa likipigania haki. Baadaye kundi hilo likaongeza maneno mengine katika kauli mbiu yao. "Turudishie haki zetu, sisi ndio wenye mamlaka!"

Joachim Gauck makes a speech after he was elected German president at Germany's Federal Assembly in Berlin, March 18, 2012. German lawmakers elected Joachim Gauck, a former Lutheran pastor and human rights activist from communist East Germany, as president of the European Union's largest country on Sunday by a large majority in a first round of voting. REUTERS/Fabian Bimmer (GERMANY - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Bundespräsidentenwahl 2012 Bundespräsident Joachim GauckPicha: Reuters

Kwa hivyo, Ujerumani imempata raisi mwanaharakati kwa dhati na imani yake. La kungoja na kuona ni ikiwa chochote kitabadilika kwa kuwapo kwake ofisini.

Mwandishi: Ute Schaeffer
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Hamidou Oummilkheir