1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaidi aliyekamatwa Italia kupelekwa Uingereza

30 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEpR

Roma:

Serikali ya Italia leo imeanza utaratibu wa kumpeleka Uingereza mtuhumiwa anayehusika na mashambulio ya mabomu mjini London aliyekamatwa mjini Roma jana Ijumaa. Polisi wakati huo huo wanaendelea kuwapeleleza watu waliowasiliana na Gaidi huyo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Giuseppe Pisanu, amesema kuwa mtuhumiwa Osman Hussain, alijaribu kutoroka wakati alipotaka kukamatwa kutokana msaada wa Waethiopia na Waeritrea wanaoishi Italia. Pisanu amesema kuwa watu wasiopungua 15 wana hojiwa. Serikali ya Uingereza imeiomba serikali ya Italia impeleke Hussain nchini humo. Polisi wa Uingereza wamewakamata watuhumiwa wengine watatu mjini London na Birmingham. Ingawaje wamefanikiwa kuwakamata Magaidi hao wamesema kuwa hata hivyo hawaondoi uwezekano wa mashambulio zaidi kufanywa mjini London.