G20 inakubali uanachama wa Umoja wa Afrika
7 Septemba 2023Kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg likivinukuu vyanzo vyenye ufahamu na suala hilo imesema, hatua hiyo itaupa umoja wa Afrika hadhi sawa na Umoja wa Ulaya.
Soma pia: Waziri mkuu wa India atoa mwito wa Umoja wa Afrika kujiunga kwenye kundi la G20
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliwaandikia viongozi waG20 mwezi Juni akipendekeza Umoja wa Afrika kujumuishwa katika kambi hiyo wakati wa mkutano wa kilele utakafanyika New Delhi, India mwishoni mwa juma.
Kwa sasa Kundi hilo linajumuisha nchi wanachama 19 na Umoja wa Ulaya.
Kundi la G20 mwaka huu pia limeyaalika mataifa 9 yasiyo wanachama yakiwemo Bangladesh, Singapore, Uhispania na Nigeria, na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.