1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Futari ya Ramadhan katika Chuo cha masomo ya juu mjini Cologne

25 Septemba 2008

Ni mkusanyiko wa waislamu na wenzao wasio Waislamu

https://p.dw.com/p/FP3r
Jamii ya Waislamu wakiwa kwenye sala katika msikiti mmoja kusini mwa Ujerumani.Picha: AP

Msikilizaji mwezi mtukufu wa Ramadhani unatarajiwa kumalizika katikati ya wiki ijayo . Kwa muda wa mwezi mzima waislamu wamo katika funga ya Ramadhani moja wapo ya nguzo tano za Uislamu.Katika chuo cha masomo ya juu mjini Cologne- Fachhochschule Köln-, kwa miaka kadhaa sasa wanafunzi wa Kiislamu hujumuika na wenzao wa dini nyengine kwa futari ya pamoja ambao kwa Waislamu huwa ni wakati wa kumaiza funga ya simu inayohusika pale jua linapokuchwa, kwa maneno mengine wakati wa Magharibi. Chakula hicho huandaliwa na jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu chuoni humo

Futari hutanguliwa na Adhana, wito wa sala ya kipindi cha Magharibi,wakati wa kufungua .Kwa Waislamu wanaotakiwa mkwa mujibu wa muongozo kusali mara tano kwa siku hiyo ni sala ya nne, pale jua linapokuchwa. Katika chuo hicho cha amasomo ya juu, Meza kubwa imeandaliwa wakiwepo karibu wanafunzi 300. Chakula ni pamoja na kuku, wali, mikate na mchuzi.

Kwa Adhana yaani wito wa sala, huwa wakati wa kufungua umewadia. Siku hiyo ni saa 1 na dakika 37 za jioni au ukipenda magharibi kwa saa za Ujerumani. Saa ya kufuturu bila shaka hubadilika kwa mujibu wa kalenda kama anavyosimulia kijana Elhakam Suni,"Bila shaka tunapata usoefu kulingana wakati wa Köln au niseme Kalenda ya Köln. Kila mji huwa na Kalenda yake. Bila shaka sio kosa kama umepitiwa dakika moja au mbili hivi. Katika Uislamu ikiwa mtu amepitiwa kwa kosa dogo kama hilo Mwenyezi Mungu anafahamu na ni mwenye kusamehe-Ishallah-Ndivyo tunavyotarajia."

Kwa miaka saba sasa hufungua pamoja wakati wa Ramadhani wanafunzi wa Kiisalamu na wasio Waislamu chuoni hapo mjini Cologne. Lakini mwanafunzi Ulrich Kock Blunk ambaye ni mkatoliki anasema kipindi kibaya katika hafla hii ya kufuturu pamoja wakati wa mwezi wa Ramadhani kilikua 2001 wakati wa shambulio la kigaidi la Septemba 11.Anaelezea hali ilivyokua akitamka kuwa,"Nafikiri kilichotokeza baada ya hali hiyo , kutokana na mazungumzo pamoja na wanafunzi wa Kiislamu ni kwamba, baada ya hujuama ya Newyork walijikuta katika hali ngumu, kupoteza ajira, kutopata nyumba za kupanga na hata kuwa na hisia kwamba watu walikua hawataki tena kuwa na mawasiliano nao. Kwa hiyo ikabidi kutafuta namna nyengine ya kuwa na mawsiliano mapya.

Vipi wanafunzi wa Kiislamu wake kwa waume wanatimiza wajibu wao wa kufunga ? Verena ni msichana wa miaka 23 ambaye si muislamu lakini hushiriki katika chakula hicho cha pamoja na wenzake wakiislamu. Anasema,"Kwenye mkahawa wa Chuoni nilikua naangalia ratiba ya chakula na ilikua nilikua mwaka a mmoja mjini Istanbul na huko pia nilishiriki katika tafrija kama hii. Huko kwa kweli siku ninafunga lakini siku moja moja nilijaribu na naona ni utamaduni mzuri na nina hisia nzuri kwa hiyo nikataka kuona hapa Ujerumani pia hali ikoje."

Kwenye meza aliyokaa Verena kuna mashoga zake wengine. Wote sita wana hijabu vichwani. Yasmin amefunga siku nzima na hiyo ni mara ya kwanza anafika katika hafla hiyo ya chakula cha pamoja kufungua funga ya Ramadhani. Yeye analiona tukio hilo la kufungua pamoja kuwa ni zuri.

Akifafanua anaeleza,"Tunasoma pamoja na wanafunzi Wakikristo na Kiislamu na wa dini nyengine pia. Wengi husikia juu ya ramadhani na funga, lakini wengi hawajui ni kitu gani. Na kwa mkusanyiko kama huu wanapata fursa ya kufahamu vizuri na hata kujenga maelewano."

Kwa Wanafunzi wengine, hii ni nafasi ya kuwa pamoja kujaza pengo la kutokusanyika pamoja na familia zao wakati huu wa Ramadhani.

Kijana Zainou kutoka Guinea mwenye umri wa miaka 27 anasema, kukaa na kufuturu peke yako kwenye chumba cha mwanafunzi ni hali ya upweke mkubwa ´na kwa maoni yake Mkusanyiko huu wa kufuturu pamoja ni mzuri, unamuondolea upweke na kumpa hamu ya kula na kukifurahi chakula.