1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fungu la 2 la msaada wa Ulaya kwa Ugiriki lapita Bungeni Berlin

28 Februari 2012

Bunge la shirikisho-Bundestag limeunga mkono mpango wa kuipatia Ugiriki fungu la pili la msaada wenye thamani ya Euro bilioni 130.Wabunge wasiopungua 7 wa kambi ya kansela hawakuunga mkono mpango huo.

https://p.dw.com/p/14BGM
Kansela Angela MerkelPicha: dapd

Kansela Angela Merkel alionekana amechoka alipopanda jukwaani bungeni .Mkononi alikamata ripoti ya serikali yake kuhusu msaada wa pili wa Ugiriki wenye thamani ya Euro bilioni 130.Katika hotuba yake bungeni kansela Angela Merkel ameelezea matumaini kwamba fedha hizo zitawekezwa ipasavyo,hata kama uvumi umeshazuka kwamba pengine fungu la tatu litahitajika.

Kansela Angela Merkel ameendelea kusema""baada ya kupima hoja za wale wanaounga mkono na wale wanaopinga,amegundua kwamba faida inayotokana na mpango huu ni kubwa kuliko hasara.

Saa tatu baadae,baada ya mjadala mkali bungeni,kansela Angela Merkel akaondoka na ushindi.Wabunge 496 wameuunga mkono,90 wamepinga na watano wamejizuwia kupiga kura.Wingi mkubwa lakini sio ule uliokuwa ukitarajiwa kutuliza hali ya mambo katika serikali ya muungano mjini Berlin.Kwasababu kile kijulikanacho kama wingi wa kura kutoka kambi ya kansela,yaani vyama shirika katika serikali kuu ya muungano mjini Berlin,haujapatikana-zilikosekana sauti saba.

Hilfspaket Griechenland Debatte Bundestag Steinbrück SPD
Peer Steinbrück wa chama cha upinzani cha SPDPicha: Reuters

Walikuwa wabunge wa vyama viwili vya upinzani,SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne waliounusuru mpango huo.Hata hivyo wawakilishi wa vyama hivyo wamesema wazi bungeni kura yao ya ndio haimaanishi wanamuunga mkono kansela Angela Merkel.Lawama za kimsingi zilitolewa.Waziri wa zamani wa fedha kutoka chama cha SPD,Peer Steinbrück ameutaja mpango huo wa kupatiwa Ugiriki fungu la pili la msaada kuwa umekawia,ni haba na si madhubuti."Hakuna mipango madhubuti ya uwekezaji" hata hivyo kutokana na wajibu wa kisiasa kwaajili ya Ulaya,kama anavyosema Peer Steinbrück,chama chake kimeunga mkono mpango huo.

"Hatutaki kumuachia yeyote aporomoke amesema kwa upande wake bibi Renate Künast wa chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne aliyependekeza paundwe mkakati maalum, wa kuiokoa Ugiriki mfano wa ule ulioandaaliwa na Marekani kwa ujerumani baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.

Hilfspaket Hilfe Griechenland Abstimmung Debatte Bundestag Gysi Die Linke
Gregor Gysi wa chama cha Die LinkePicha: dapd

Chama pekee cha upinzani ambacho hakijaunga mkono mpango huo ni-Die Linke.Mkuu wa chama ahicho bungeni Gregor Gysi alizusha ghadhabu bungeni alipolinganisha masharti ya kupatiwa msaada Ugiriki na yale ya kulipa fidia yaliyotolewa kwa Ujerumani baada ya vita vikuu vya kwanza vya dunia.

Mwandishi:Kiesel Heiner (DW Berlin)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri Yusuf Saumu