1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Freetown. Kazi ya kuhesabu kura yaendelea.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZY

Kazi ya kuhesabu kura inaendelea nchini Sierra Leone baada ya uchaguzi wake wa kwanza tangu majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa kuondoka nchini humo miaka miwili iliyopita.

Matokeo ya mwanzo yanaonyesha kuwa huenda ikahitajika duru ya pili ili kumpata rais mpya wa nchi hiyo.

Wapiga kura wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya uchaguzi wa Jumamosi, unaoonekana kama mtihani kwa uthabiti wa taifa hilo la Afrika magharibi baada ya miaka 11 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati huo huo , mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana ameusifu uchaguzi huo nchini Sierra Leone na kuahidi kuwa umoja huo utaendelea kuliunga mkono taifa hilo la Afrika magharibi.Solana amesema mjini Brussels kuwa uongozi mpya wa nchi hiyo unapaswa kusaidia nchi hiyo kusonga mbele kisiasa na kiuchumi na umoja wa Ulaya utasaidia.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa katika muda wa wiki mbili zijazo.