1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT

16 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFdO

Shirikisho la mchezo wa soka la Ujerumani limetangaza kuwa mechi moja ambayo ilichezwa katika mazingira ya kashfa ya kupanga matokeo itarudiwa kuchezwa.Hii itakuwa ni mara ya kwanza jambo kama hili kutokea katika soka ya Ujerumani.

Mechi hiyo iliyotiliwa mashaka ni ile iliyochezwa mwaka jana,iliyovikutanisha vilabu vya daraja la pili vya Ahlen na Burghausen na kuchezeshwa na mwamuzi Robert Hoyzer,ambae anakabiliwa na mashtaka ya kuchezesha mechi alizopanga matokeo,huku akiwa amecheza kamari juu ya matokeo ya mechi hizo.

Hoyzer ambaye kwa hivi sasa yupo kizuizini,amewaambia waendesha mashtaka kuwa alikuwa na ushawishi wa matokeo ya mechi hiyo pamoja mechi nyingine.

Katika muendelezo wa kashfa hiyo,Shrikisho hilo la Soka la Ujerumani limemsimamsha mwamuzi mwengine ambaye ametajwa na Hoyzer kuwa nae alishiriki katika kashfa hiyo.Mwamuzi huyo Dominik Marks anatuhumiwa kupokea euro 36,000 kwa ajili ya kupanga matokeo ya mchezo wa soka.