1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT : Rais Köhler ashambuliwa

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fj

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameshambuliwa lakini hakujeruhiwa hapo jana wakati akiondoka kwenye sherehe za kumtunuku tuzo mtaalamu wa historia wa Israel Saul Friedlaender kwa uandishi wake juu ya maangamizi ya Wayahudi.

Mtu mwenye umri wa miaka 44 alimvamia Köhler wakati akiondoka kutoka kanisani kwa kuzinyaka kosi za koti lake kabla ya kudhibtiwa na walinzi.

Manfred Vonhausen msemaji wa polisi mjini Frankfurt amesema kutoka kwenye umma wa watu mtu mmoja alikurupuka kwa ghafla na kujaribu kumshambulia rais na alifanikiwa kwa muda mfupi kumnyaka rais kwa nyuma lakini papo hapo maafisa wa ulinzi walimzidi nguvu na kumdhibiti.

Köhler na mke wake walikuwa wakiondoka kutoka sherehe hizo katika kanisa la St.Paul wakiwa pamoja na Friedlaender wakati mtu huyo wa asili ya Romania ambaye anaishi katika mji ulio karibu wa Offenbach alipomvamia rais.

Polisi imesema mtu huyo ameachiliwa huru baada ya kuhojiwa na kwamba alikuwa ameonekana kuchanganyikiwa akili.

Rais Köhler wa Ujerumani alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima kanisani ambapo kwa kawaida tuzo hiyo ya amani yenye hadhi ya wachapisha vitabu wa Ujerumani hutolewa katika siku ya mwisho ya Maonyesho ya Vitabu ya Frankfurt ambayo ni makubwa kabisa duniani.