Frankfurt. Mturuki apata tuzo ya vitabu.
24 Oktoba 2005Mwandishi vitabu wa Uturuki Ohran Pamuk amepata tuzo ya yenye hadhi ya juu ya biashara ya vitabu nchini Ujerumani ya amani.
Mwandishi huyo wa vitabu ambavyo ni pamoja na vitabu maarufu vya Snow na My Name is Red, amesema katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo kuwa kujihusisha katika siasa ni sehemu ya kawaida kwa mwandishi.
Chama cha wauza vitabu nchini Ujerumani kimemsifu Pamuk kwa kujenga daraja kati ya mashariki na magharibi. Pamuk amerudia uungaji mkono wake kwa juhudi za Uturuki kujiunga na umoja wa Ulaya , akisema kuwa ni muhimu kwa ajili ya amani katika eneo hilo na maelewano kati ya tamaduni. Tuzo hiyo inatolewa kila mwaka na kuingiliana na sherehe za maonyesho ya vitabu ya Frankfurt, ambayo yamemalizika hivi karibuni.