FRANKFURT: Motassadeq atafikisha kesi yake mbele ya mahakama ya juu kabisa
19 Novemba 2006Matangazo
Mmorokko aliekutikana na hatia ya kuwasaidia marubani waliojitolea muhanga katika mashambulio ya Septemba 11,atakata rufaa katika mahakama ya juu kabisa nchini Ujerumani.Siku ya Alkhamisi, katika mahakama ya rufaa,Mounir el-Motassadeq ambae tayari anakabiliwa na kifungo cha miaka saba kwa makosa ya kuwa mwanachama katika kundi la kigaidi,tena alikutikana na makosa mengine 246 ya kuhusika na mauaji.Mwanasheria Ladislav Anisic anaemtetea Motassadeq aliekanusha kujua habari za mashambulio yaliopangwa kufanywa mwaka 2001 amesema,Motassadeq ataifikisha kesi yake mbele ya Mahakama ya Katiba ya Ujerumani.