FRANKFURT: Misafara ya ndege ya Airbus A380
17 Machi 2007Matangazo
Ndege ya abiria iliyo kubwa kabisa duniani,ya shirika la Airbus-A380,imetua kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani kuanza mlolongo wa safari za majeribio.Siku ya Jumatatu ndege hiyo,chini ya jina la shirika la ndege la Kijerumani-Lufthansa itafanya safari yake ya kwanza kwenda New York ikiwa na kama abiria 500. Safari zingine kwenda Hongkong,Washington na Munich zitaanzia pia uwanja wa ndege wa Frankfurt.Misafara hii inafanywa na Airbus na Lufthansa ili kuweza kuichunguza ndege hiyo mpya, katika hali halisi zinazokutikana wakati wa kusafiri.