1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frankfurt. Masoko ya hisa yapata faida.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOU

Masoko ya hisa katika mataifa ya Asia na Ulaya yamepanda kutokana na kupunguzwa jana Jumanne kwa viwango vya riba nchini Marekani na benki kuu ya nchi hiyo. Nchi hiyo imepunguza viwango vyake vya riba kwa kiasi cha nusu ya asilimia na kufikia asilimia 4.75 ili kuzuwia athari za mzozo wa mikopo ya nyumba nchini Marekani.

Hisa nchini Japan zimeongezeka kwa asilimia 3.7 katika soko la hisa la Nikkei, ikiwa ni ongezeko kubwa kabisa kwa siku nchini humo katika muda wa miaka mitano. Mataifa mengine ya bara la Asia yalifuata mkumbo huo, ikiwa soko la hisa la India limepanda kwa asilimia 2.5.

Katika bara la Ulaya masoko ya hisa pia yamepata faida , ikiwa soko la hisa mjini London , Frankfurt na Paris yakipata kiasi cha asilimia 2 mara baada ya kufunguliwa masoko hayo leo Jumatano.

Sarafu ya Euro inauzwa kwa kiwango cha juu kipya cha dola moja na senti 39 kwa Euro moja.