1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT : Benki Kuu zamiminia fedha mfumo wa benki

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaL

Benki Kuu za Ulaya na Hazina ya Marekani zimemimina mabilioni kwenye mfumo wa fedha kwa siku ya pili mfululizo kuepusha matatizo makubwa ya mikopo duniani.

Hatua hiyo inafuatia hatua kama hizo zilichokuliwa na mabenki ya Asia.Masoko yaliyumba kutokana na taarifa za matatizo kwenye mabenki na michango ya fedha kulikotokana na uwekezaji wa kuhatarisha kwenye masoko ya ukopeshaji ya nyumba na mali nchini Marekani na kuzusha hofu ya kukatwa kwa mikopo nafuu ambayo imekuwa ikichochea ukuaji wa uchumi duniani.

Benki zimechukuwa hatua hiyo kuhakikisha kuna michango ya kutosha kuwezesha masoko ya fedha yafanye kazi kwa utulivu na kuzuwiya kupanda kwa ghafla kwa viwango vya riba vya muda mfupi.