Mkuu wa mkoa wa zamani huko Rwanda ashitakiwa Ufaransa
23 Septemba 2023Matangazo
Chanzo kutoka mamlaka hizo kinasema kuwa Pierre Kayondo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kibuye na pia mbunge wa zamani, alikamatwa Jumanne iliyopita na kushitakiwa hapo hapo kwa kushiriki kwenye mauaji ya maangamizi na uhalifu dhidi ya ubinaadamu na tangu wakati huo yuko mahabusu.Kayondo alikuwa anachunguzwa na mamlaka za Ufaransa tangu mwaka 2021 baada ya jumuiya moja ya wahanga wa mauaji hayo kufunguwa mashitaka dhidi yake.Inaaminika alikuwa akiishi kwenye mji wa kaskazini mwa Ufaransa wa Le Havre. Ufaransa imekuwa kimbilio kubwa la watuhumiwa wanaokwepa kukamatwa kwa ushiriki wao kwenye mauaji ya zaidi ya watu laki nane, wengi wao kutoka jamii ya Watutsi waliouawa ndani ya kipindi cha siku 100 tu nchini Rwanda.