1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fischer: Mkutano wa Afghanistan kuzungumza madawa ya kulevya

27 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFeD
BERLIN: Kupigwa vita biashara ya madawa ya kulevya itakuwa mojawapo ya mada za mbele kabisa katika Mkutano wa Afghanistan mjini Berlin aliarifu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Joschka Fischer. Jamii ya Kimataifa itapaswa kuongeza juhudi zake katika sekta hii, alisisitiza Bwana Fischer wakati akizungumza na TV ya DEUTSCHE WELLE. Alisisitiza kuwa katika uhusiano huo Ujerumani imetekeleza ahadi yake ya misaada ya fedha iliyotoa katika mikutano ya mataifa fadhili. Pia nchi nyingine zitapaswa kutekeleza ahadi zao. Ustawi wa uchumi wa Afghanistan pamoja na kuendelezwa mifumo yake ya elimu na afya ni miongoni mwa mambo muhimu katika kupigana na ugaidi, alisema mwana-siasa huyo wa chama cha Mazingira. Mkutano wa Afghanistan unaoanza Jumatano inayo utahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 65.