FIFA: Nusu ya watu duniani waliangalia kombe la dunia 2018
21 Desemba 2018FIFA imesema uhakiki uliofanywa na kampuni ya Publicis Media Sport and Intertainment of World Cup utazamaji ulionesha kwamba watu bilioni 3.572 waliatazama kakriban baadhi ya matukio ya mashindano hayo kuanzia Juni 14 hadi Julai 15 katika televisheni nyumbani kwao, katika majukwaa ya kidigitali, maeneo ya wazi ya umma ama katika mabaa na mikahawa.
Ripoti hiyo inasema tarakimu hizo zinawakilisha asilimia 51.3 ya watu wote duniani wenye umri wa miaka kuanzia minne na zaidi. Fainali kati ya Ufaransa na Croatia ilishuhudia watu bilioni 1.2 wakiangalia kwa takriban hata dakika moja tu.
FIFA imesema ripoti hiyo inaonesha kwamba kwa muda wa utazamaji wa wastani umepanda ikilinganishwa na fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil mwaka 2014, ambapo watu bilioni 2.49 walitazama mashindano hayo kwa takriban dakika 30, ikiwa ni juu kutoka watu bilioni 1.95 miaka minne iliyopita.
Wastani wa kati wa utazamaji kwa kila mchezo kati ya michezo 64 ilikuwa watu milioni 191, ikiwa ni ongezeko kutoka watu milioni 187 mwaka 2014 nchini Brazil, FIFA limesema , "kila mchezo ulikuwa ni tukio la televisheni duniani katika kiwango chake."
Lakini watu walioshuhudia mchezo moja kwa moja kwa ajili ya fainali ilishuka kwa asilimia 5.1 na ule wa nusu fainali ulipukuwa chini ya asilimia 15.5 kuliko mwaka 2014 ambapo uhakiki umesema kwamba sababu ni pamoja na uchache wa idadi ya watu katika nchi zilizohusika na ni shirikisho moja tu lililowakilishwa , yaani shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA katika timu nne za nusu fainali katika fainali hizo za Urusi. Awamu ya makundi na timu bora zilizoingia katika awamu ya timu 16 utazamaji ulipanda kwa ulinganisho.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae