Fernandes "hana nyota ya unahodha"
30 Oktoba 2023Kauli hii ni kulingana na mchezaji wa zamani Roy Keane, ambaye amemkashifu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno baada ya United kupoteza 3-0 dhidi ya Manchester City jana Jumapili.
Keane, nahodha wa zamani wa United, aliunga mkono maneno ya mchezaji mwengine wa zamani Gary Neville ambaye alisema baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 7-0 na Liverpool msimu uliopita, kipigo kikubwa zaidi tangu 1931.
Neville amesema baadhi ya tabia ambazo alionyesha Fernandes katika kipindi cha pili ni "aibu."
Fernandes alichukua unahodha msimu uliopita baada ya Harry Maguire kuvuliwa nafasi hiyo.
Katika mechi hiyo ErlingHaaland alicheka na wavu mara mbili kisha Phil Foden akagongelea msumari wa mwisho kwa bao la tatu na kuwafanya vijana wa Pep Guardiola kuwa pointi tisa zaidi ya United katika jumla ya mechi 10 msimu huu.