1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fedha za serikali ya Gaddafi kuwasaidia waasi

5 Mei 2011

Mkutano wa kundi la kimataifa kuhusu Libya, umetangaza kuanzisha mfuko maalum wa fedha kuwasaidia waasi wa Libya wanaopambana na serikali ya Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/RMEs
Der italienischen Außenminister Franco Frattini (r) und der Premier von Katar, Scheich Hamad bin Jassim bin Jabor Al-Thani scherzen am Donnerstag (05.05.2011) im Außenministerium in Rom während eines Termins für ein Gruppenfoto. Links stehen US-Außenministerin Hilary Clinton der französische Außenminister Alain Juppe. In Rom findet das Treffen der internationale Libyen-Kontaktgruppe statt, welche die Suche nach einer politischen Lösung für das nordafrikanische Land vorantreiben will. An den Beratungen nehmen die Vertreter von insgesamt 40 Staaten und internationalen Organisationen teil. Foto: Hannibal dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Viongozi waliohudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu Libya mjini RomePicha: AP

Tangazo hilo limetolewa hii leo katika hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Franco Frattini alieongoza mkutano huo pamoja na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa al Thani, mjini Rome. Waziri Frattini amesema, mfuko huo ulioitwa "Utaratibu wa Fedha wa Mpito" utaruhusu kulisaidi kundi kuu la upinzani ITNC, nchini Libya kwa ufanisi na uwazi. Kundi hilo lenye makao yake mjini Benghazi, limesema linahitaji kati ya dola bilioni 2 hadi bilioni 3 kuendesha operesheni zake dhidi ya vikosi vya Gaddafi. Ripoti zinasema kuwa Umoja wa Ulaya na Marekani zimezuia kiasi ya Euro bilioni 40 za serikali ya Libya katika benki za kigeni.

Nguvu za kijeshi kuishinikiza serikali ya Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton aliehotubia mkutano wa waandishi wa habari pamoja na waziri mwenzake wa Italia Franco Frattini, ameahidi kuwa serikali mjini Washington itatumia mali ya serikali ya Muammar Gaddafi, iliyozuiliwa nchini Marekani. Wakati huo huo Frattini amesema kuwa Italia na Marekani zinaamini kuwa nguvu za kijeshi kama mashambulio ya anga yanayofanywa na NATO hivi sasa ni njia pekee ya kuishinikiza serikali ya Gaddafi kusita kuwashambulia raia nchini Libya. Nae waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle alipozungumza kuhusu kiongozi wa Libya Gaddafi, kabla ya mkutano huo wa Rome alisema:

"Yeye ameanzisha vita dhidi ya nchi yake mwenyewe. Vile vile hajizui kutenda ukatili, kwa hivyo ni muhimu kabisa kukomesha mapigano hayo na ukatili unaofanywa. "

Muhimu kutafuta ufumbuzi wa kisiasa

Außenminister Guido Westerwelle (FDP) nimmt am Donnerstag (05.05.2011) im Außenministerium in Rom an dem Treffen der internationale Libyen-Kontaktgruppe teil, welche die Suche nach einer politischen Lösung für das nordafrikanische Land vorantreiben will. An den Beratungen nehmen die Vertreter von insgesamt 40 Staaten und internationalen Organisationen teil. Foto: Hannibal dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: picture-alliance/dpa

Lakini, Westerwelle vile vile amesisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho la kisiasa katika mzozo wa Libya. Wakati huo huo, waziri wa nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglo ametoa mwito wa kusitisha mapigano nchini Libya katika muda wa siku saba.

Mkutano wa Rome umehudhuriwa na Marekani, nchi za Ulaya zinazoshiriki katika operesheni ya NATO dhidi ya Libya, washirika kutoka Mashariki ya Kati na mashirika ya kimataifa, huku mapigano makali yakiripotiwa ndani na ukingoni mwa mji wa Misrata.

Zaidi ya Walibya na wageni 1,000 wamehamishwa kutoka Misrata na wamewasili Benghazi kwa meli iliyokodiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji ili kuwasaidia wafanyakazi wa kigeni kutoka nchi za Kiafrika.

Mji wa Misrata umezingirwa na vikosi vya Gaddafi kwa zaidi ya miezi miwili huku waasi na vikosi vya serikali vipigana vikali ili kuudhibiti mji huo wa bandari.

Mwandishi: Martin,Prema/RTRE,AFPE,DPAE

Mhariri:Josephat Charo