FC Bayern yapigwa mabao 4 na Real Madrid
30 Aprili 2014Matangazo
Real Madrid waliwacharaza wenyeji wao kupitia mabao yaliyofungwa na Sergio Ramos aliyefunga mabao mawili ya kichwa kabla ya mchezaji mahiri Christiano Ronaldo kuifungia Real mabao mengine mawili na kudidimiza ndoto ya Bayern Munich ambao ni mabingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga. Huko katika eneo la Bayern kulikopigwa kipute Sudi Mnette amezungumza na Mdau wa Soka Salim Malumbo, kwanzaailitaka kujua anazungumziaje kipigo hicho? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo