Nkem Begho wa mjini Lagos nchini Nigeria, hakuweza kufanikiwa kupata nguo zinazofaa kwa ajili ya watoto. Kwa kuwa hakuweza kuridhika na nguo alizoziona, aliamua kubuni chapa ya nguo zake zenye asili ya kiafrika. Lengo ni kuwa na nguo mahsusi ambazo pia zinaweza kutambulisha utamaduni wa Nigeria.