Chama cha siasa kali chatajwa kushindwa Uholanzi
23 Novemba 2023Habari hizo ni bomu la kisiasa ambalo litaitikisa Ulaya na kote ulimwenguni. Chama chake cha Uhuru, PVV kimeshinda viti 35 bungeni, ikiwa ni ushindi wa kishindo kwa mujibu wa matokeo ya awali na pia maoni ya waliopiga kura. Kundi la siasa za mrengo wa kushoto linafuata na viti 25, huku chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia kikiwa na viti 24. Iwapo itathibitishwa, ushindi wa Wilders unadhihirisha mabadiliko ya ghafla ya siasa za mrengo wa kulia kwa taifa hilo la tano kwa ukubwa la Umoja wa Ulaya, na utapokelewa kwa hofu katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels. Chama cha PVV kimeahidi kura ya maoni kuhusu uwanachama wa Uholanzi katika Umoja wa Ulaya. Licha ya ushindi huo wa uchaguzi, haijawa wazi ni vipi Wilders anaweza kupata uungwaji mkono wa kutosha kutengeneza muungano mpana ili kuunda serikali imara.