UchumiKimataifa
FAO: Bei ya vyakula duniani ilishuka mnamo mwaka 2023
5 Januari 2024Matangazo
Shirika hilo lenye makao makuu yake mjini Rome Italia limeeleza kuwa, bei ya bidhaa za chakula duniani ilishuka kwa asilimia 13.7 mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022.
Hata hivyo, bei ya sukari tofauti na bidhaa nyengine, ilipanda kwa asilimia 26.7 mwaka jana japo ilishuka tena mwezi Disemba hasa baada ya Brazil kuongeza usafirishaji wa mauzo yake ya nje.
Faharasa ya bei ya chakula ya FAO hufuatilia bei za soko la kimataifa za vyakula vikuu vitano vinavyotumika zaidi duniani.