1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNepal

Familia zakabidhiwa miili ya waliokufa katika ajali ya Nepal

17 Januari 2023

Hospitali nchini Nepal imeanza zoezi la kuikabidhi miili ya waliouawa katika ajali ya ndege kwa familia zinazoomboleza. Watu 72 walikufa katika ajali ya ndege iliyotokea Jumapili

https://p.dw.com/p/4MIMP
Nepal | Flugzeugabsturz
Picha: Yunish Gurung/AP Photo/picture alliance

Wafanyakazi wa uokozi wamekuwa wakifanya kazi bila kupumzika, kuitafuta miili ya marehemu kutoka vipande vya ndege hiyo ilioanguka kwenye korongo na kisha kuwaka moto. Inaminika kuwa watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo; wasafiri 68 na wafanyakazi wanne, walipoteza maisha.

Watoto sita na raia 15 wa kigeni ni miongoni mwa wahanga hao. Afisa wa polisi ameliarifu shirika la habari la AFP kuwa hadi mapema leo miili sabini ilikuwa imekwishapatikana.