Rais Uhuru Kenyatta na mama yake wametajwa na nyaraka hizo kuwa kumiliki akaunti za siri Panama, huku ndugu zake watatu wakimiliki kampuni tano za nje ya nchi zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 30. Lakini si Kenyatta wala familia yake waliotoa ushirikiano kwa timu ya uchunguzi huo uliofanywa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ) na vituo 150 vya habari vya kimataifa.