1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fainali ya Kombe la Ujerumani; Leipzig na Dortmund

13 Mei 2021

Fainali ya 78 ya Kombe la Ujerumani itawakutanisha RB Leipzig na Borussia Dortmund kupambana katika Uwanja wa Olimpiki huko Berlin Leo Alhamisi. Je! Nagelsmann ataingoza Leipzig kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza?

https://p.dw.com/p/3tLiy
Vorschau DFB Pokalfinale RB Leipzig - Borussia Dortmund
Picha: Waelischmiller/Hoermann/SVEN SIMON/imago images

Fainali ya 78 ya Kombe la Ujerumani itawakutanisha RB Leipzig na Borussia Dortmund kupambana katika Uwanja wa Olimpiki huko Berlin Leo Alhamisi. Je! Julian Nagelsmann atamwongoza Leipzig kutwaa xtaji hilo kwa mara ya kwanza? Soma zaidi BVB mabingwa wa kombe la Ujerumani

RB Leipzig inaweza kuwa mshindi wa 26 tofauti wa mashindano ya kombe la Ujerumani ikiwa wataweta kubadilisha jaribio lao la awali wakati walipoteza 3-0 dhidi ya Bayern Munich mnamo 2019.

Deutschland Bundesliga RB Leipzig vs TSG Hoffenheim
Yussuf Poulsen mchezaji wa RB Leipzig Picha: Revierfoto/imago images

Mshambuliaji wa RB Leipzig Yousef Polsen kupitia mtandao wake wa twitter amendika kuwa "Mechi hii ina umuhimu mkubwa sana kwetu".

Borussia Dortmund wamefuzu kwa fainali ya Kombe la Ujerumani mara 10, na kushinda taji hilo mara nne, hivi karibuni miaka minne iliyopita dhidi ya Eintracht Frankfurt (2-1). Ushindi dhidi ya Leipzig utakua wa tano wa kombe la Ujerumani na kuwaweka sawa na wapinzani wao FC Schalke 04 na Eintracht Frankfurt katika nafasi ya tatu kwa mataji mengi ya Kombe la Ujerumani.

"Ni wazi mchezo wa leo ni muhimu na itakuwa na mhemko kwangu. Kusema hivyo, bado tuna michezo miwili iliyobaki katika Bundesliga, ambayo tuna matumaini makubwa. Ningefurahi sana ikiwa ningeweza kuaga Leipzig na kombe la Pokal na ushindi mara mbili katika mechi mbili za Bundesliga. Nina matumaini mazuri mbele ya mchezo wa leo na nahisi wachezaji wana hisia mchanganyiko na msisimko kabla ya fainali. Tunajivunia sana kuwa tumetinga fainali ." Amesema Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann. Soma zaidi Bayern sasa wamtaka Nagelsmann

Borussia Dortmund watalazimika kusubiri iwapo mshambuliaji nyota Erling Braut Haaland atakuwa imara kimchezo baada ya kuwa nje kutokana na jeraha.   soma zaidi Haaland aizima RB Leipzig

Deutschland Bundesliga RB Leipzig - Borussia Dortmund
Picha: Ronny Hartman/REUTERS

Haaland amecheka na wavu mara 37 katika mechi 38 alizoichezea Dortmund msimu huu. Ajenti wa Mshambuliaji huyo ameashiria kuwa huenda Haaland akaondoka Dortmund mwishoni mwa msimu huu iwapo Dortmund walio katika nafasi ya nne katika jedwali la Bundesliga watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. soma Kinyang'anyiro cha Bundesliga chashika kasi

Leipzig wanashuka dimbani bila ya Kiungo wa Tyler Adams na beki wa kushoto  Angelinho.

Huenda timu hizi zikatumia wachezaji hawa katika vikosi vyao:

Kikosi : Leipzig

Gulasci – Klostermann, Upamecano, Orban – Mukiele, Kampl, Sabitzer, Laimer – Olmo, Haidara – Poulsen

Kikosi : Dortmund

Bürki – Piszczek, Akanji, Hummels, Guerreiro – Can, Dahoud, Bellingham – Reus, Sancho – Haaland

     

Vyanzo; AFP, https://p.dw.com/p/3tK5m