Fainali ya kombe la DFB kwa soka la wanawake Ujerumani
25 Machi 2011Matangazo
Mpaka siku ya Alhamisi tiketi elfu 17 kwa ajili fainali hiyo zilikuwa zimekwishanunuliwa. Turbine Potsdam wanajiwinda kushinda kombe la pili baada ya wiki iliyopita kutwaa ubingwa wa bundesliga, katika fainali iliyoudhuriwa na Rais wa Ujerumani Christian Wulff.
Meya wa jiji la Cologne Jürgen Roters amesema fainali hiyo itakuwa ni ya kusisimua na mwangaza wa soka la wanawake nchini Ujerumani kuelekea fainali za dunia za wanawake ambazo zitafanyika hapa Ujerumani mwezi wa sita mwaka huu.
Meneja wa FFC Frankfurt Siegfried Dietrich amesema fainali hiyo ni ndoto kwao.Naye kocha wao Sven Kahlert amesema msimu huu umekuwa wa kusisimua sana kwao.Amesema wameonesha kandanda zuri.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA
Mhariri:Othman Miraji