1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fainali ya FA kubatizwa jina la "Heads up" kwa afya ya akili

Sekione Kitojo
12 Juni 2020

Fainali ya  kombe  la  FA nchini Uingereza itabatizwa jina la  fainali ya  "Heads Up FA"  ikiwa  na  nia  ya  kuonesha umuhimu wa  afya ya  akili duniani, amesema  mwanamfalme William .

https://p.dw.com/p/3dfbo
FA Cup Gewinn FC Arsenal 17.05.2014 Fabianski & Mertesacker
Picha: Reuters

Fainali  ya  kombe  la  FA  nchini  Uingereza  itafanyika  katika uwanja  maarufu  wa  Wembley  katika  tarehe  iliyobadilishwa  ya Agosti 1,  baada  ya  janga  la  virusi  vya  corona  kulazimisha kusitishwa  kwa  mipango  yote  ya  mchezo  wa  kandanda.

Shirika  la  andege  lenye  makao  yake  makuu  mjini  Dubai limekuwa  likifadhili  mashindano  hayo  ya  kihistoria  tangu mwaka 2015 lakini  limekubaliana  na  mabadiliko  hayo  ya  jina kwa  ombi la  mwanamfalme  William , ambae  pia  ni  anatumika  kama  rais wa  shirikisho  la  kandanda  la Uingereza FA.

England Prinz William Royal Baby
Mwanamfalme William wa UingerezaPicha: picture-alliance/dpa/AP Photo/C. Wigglesworth

Mwanamfalme  William  alisema  juhudi  hizo  zitakuwa "wakati  wa kuhimiza mambo  mazuri, afya chanya  ya  akili kwa  kila  mtu."

"Ni muda  muafaka  ikizingatiwa  kwamba  wote tumekwenda  pamoja katika  janga  hili," ameongeza  mwanamfalme  huyo wa Cambridge.

"Nafikiri kutakuwa, kwa masikitiko , mambo  mengi  yatakayojitokeza kutokana  na  hili  katika  jamii, sio tu  katika mchezo  wa  mpira, kwa mintarafu  ya  afya  ya  akili  ya  watu.

Fußball Pokal England Chelsea v Manchester United - Emirates FA Cup - Final - Wembley Stadium
Fainali ya kombe la AF kati ya Chelsea na Manchester United tarehe 19.05.2018Picha: picture-alliance/empics/N. Potts

"Ni  matumaini  kwamba  Kombe  la  FA  litakuwa  nguzo  ambayo inaweza watu  wanaweza  kuitegemea."

Michuano  ya  kombe  la  FA itaanza  tena  katika  awamu ya robo fainali  mwishoni  mwa  juma kuanzia  Juni 27-28.