Euro yapanda dhidi ya dola ya Marekani.
27 Februari 2008Sarafu ya euro imepanda kwa kiwango cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa hata sasa dhidi ya dola ya Marekani.Wachambuzi wanasema euro ilipata msukumo kutokana na hali bora zaidi ya biashara nchini Ujerumani kuliko ilivyotarajiwa awali.
Kupanda mno kwa sarafu ya euro kumezusha shinikizo kwa uchumi wa Marekani na kuna ripoti kwamba huenda idara ya hazina ya Marekani ikalazimika kupunguza viwango vya riba.
wafanya biashara wanaendelaea kutathimini hali ya kiuchumi kwa wakati huu baada ya dola kuanguka vibaya katika soko la fedha la New York huku baadhi ya wataalamu wakibashiri juu ya uwezekano wa kuzuka msuko suko wa kiuchumi nchini Marekani.
Utafiti unaashiria kwamba imani ya wanunuzi nchini Marekani imeshuka, imeanguka kufikia kiwango cha chini kabisa tangu Novemba 1993.
Kupanda kwa kiwango cha sarafu ya euro hadi kufikia euro moja kwa dola moja na nusu, kunavuka kiwango cha Novemba 23 mwaka jana ilipofikia dola moja nukta 4967.
Idara ya kazi ya Marekani imesema mfumko wa bei pia katika biashara ya jumla ilipanga bila kutarajiwa mwezi Januari kwa moja asili mia kwa sababu ya kupanda bei ya chakula na nishati.
Kupanda kwa chakula ana nishati na hasa bei ya mafuta yasiosafishwa kulisababisha bei za bidhaa kupanda hadi 7.4 asili mia nchini Marekani katika kipindi cha miezi 12 iliopita hadi kufikia Januari mwaka huu.
Wafanya biashara wanasema bajeti ya Marekani na nakisi katika sekta ya biashara pia ni mambo yanayohujumu uimara wa sarafu ya dola,ingawa ripoti za karibuni zinaonyesha udhaidu wa dola unatoa msukumo fulani kwa bidhaa za Marekani zinazosafirishwa n´gambo.
Washiriki katika shughuli za masoko wanasema kinyume na ilivyotarajiwa, ripoti za hali ya biashara kwa jumla nchini Ujerumani imeasaidia kuimarisha sarafu ya euro.
Wanauchumi wengi wanaamini kwamba ishara ya kwamba uchumi wa eneo linalotumia sarafu ya euro unaendelea kuwa katika hali ya kukua, itaituhusu Benki kuu ya ulaya kuendelea na kiwango cha sasa cha 4 asili mia kwa muda, na kujiepusha na uwezekano wa kupunguzwa viwango vya riba.
Hata hivyo kupanda kwa euro huenda kwa mara nyengine tena kukuzusha wasi wasi juu ya athari za kuwa na euro imara mno kwa bidhaa muhimu zinazosafirishwa n´gambo kutoka nchi za eneo la matumizi ya sarafu hiyo ya euro.