1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro 2016: sasa ni hatua ya mchujo

24 Juni 2016

Dimba la ubingwa wa Ulaya – Euro 2016 limeingia katika hatua kali na inayotarajiwa kusisimua zaidi. Hatua ya mchujo. Lakini vipi mambo yamekuwa hadi kufikia sasa, hasa katika michuano ya hatua ya makundi?

https://p.dw.com/p/1JCbF
Frankreich Fußball-EM Spanien vs. Kroatien Nikola Kalinic Tor
Picha: Reuters/S. Perez

Timu zilizopigiwa upatu zilionekana kuyumba, timu zilizoonekana kuwa ndogo zilijiamini, na idadi ndogo ya mabao yaliyofungwa iliyafanya mabao ya kufungwa katika dakika za mwisho kuwa na thamani zaidi.

Kabla ya dimba kuanza, kwa kutegemea yeyote uliyemuuliza, Ujerumani, Ufaransa, Uhispania na hata Ubelgiji zilipigiwa upatu kushinda taji la mwaka huu. Baada ya wiki mbili, kama ilivyotarajiwa, timu hizo zote ziliponea kufuzu katika hatua ya makundi, lakini kusema kweli, hakuna timu iliyoonyesha wazi kuwa itakuwa ngumu kushindwa na mpinzani.

Ujerumani na Ufaransa zimekuwa mbovu katika safu ya mashambulizi. Mchezaji wa Ujerumani ambaye kawaida hutegemewa sana Thomas Müller, hajaonekana sana. Uhispania na Ubelgiji zimeonekana kuwa na matatizo katika idara ya ulinzi licha ya kuwa na wawili kati ya makipa mahiri zaidi barani Ulaya. Ni Italia ambayo imeonekana kuridhisha, kando na mchuano wa Jamhuri ya Ireland ambao haukuwa na umuhimu sana kwao.

UEFA EURO 2016 - Island vs. Österreich *** Freistoß Alaba
Iceland ilifuzu katika hatua ya mtoanoPicha: Reuters/D. Staples

Timu ndogo zinatamba

Timu ndogo zimeonekana kufanya vyema, na inastahili kuwapigia makofi ya pongezi Ireland ya Kaskazini Iceland na Hungary kwa kutinga hatua ya mtoano. Lakini nini imekuwa siri ya timu hizi ndogo? Zote zina kitu kimoja: hazina wachezaji nyota. Zote zinasisitiza kucheza kama timu kwa sababu hazina chaguo jingine. Baadhi ya wachezaji nyota wa timu kubwa wanaonekana kuchoka kutokana na uchovu wa msimu wa kandanda la ligi zao za ndani.

Mabao machache

Mabao yamekuwa machache kutokana na timu kuimarisha safu zao za ulinzi. Huenda mtu akasema hakuna mabao mengi kwa sababu baadhi ya nchi zinacheza bila ya washambuliaji nyota, baada ya dimba hilo la euro kuongeza kwa timu nane zaidi idadi ya timu zinazoshiriki. Labda timu zinacheza kwa kujikinga zaidi na kuhakikisha kuwa zinamaliza katika nafasi ya tatu badala ya kutafuta ushindi na mwishowe kuduwazwa kwa kuwa mojawapo ya timu nane zilizobanduliwa nje baada ya duru ya kwanza. Lakini pia mabao machache yaliyofungwa, mengi yamepatikana katika dakika za mwisho mwisho. Haijulikani ni kwa nini lakini huenda uchovu wa wachezaji unachangia

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu