Euro 2016 kuandaliwa chini ya ulinzi mkali
28 Machi 2016Valls amesema maeneo ya umma ambayo mashabiki watakusnyika kuangalia michuano kwenye skrini kubwa yatakuwa chini ya ulinzi mkali, kama tu itakavyokuwa ndani ya viwanja vitakavyoandaa michuano hiyo "tunatarajia watu 7,000 hadi 8,000 wakati wa dimba la euro, na hiyo pekee ni katika maeneo ya mashabiki. Maeneo haya, tumejadiliana na Waziri wa mambo ya ndani Benard Cazeneueve na mameya wote na pia rais wa miji inayoandaa euro, Alain Juppe, kuhakikisha kuwa usalama unawekwa, na idadi sawa ya polisi, mbinu sawa na zile zitakazowekwa viwanjani. Hii ina maana kuwa maeneo fulani yatafungwa na kutakuwa na upekuzi wa mabegi
Mashambulizi ya Novemba 13 yaliyalenga maeneo ya burudani mjini Paris na kuwauwa watu 130. Walipuaji watatu wa kujitoa mhanga walijilipua nje ya uwanja wa mpira wa Stade de France, uwanja utakaoandaa mchuano wa ufunguzi wa Euro 2016, fainali na michuano mingine mitano. Takribani mashabiki milioni 2.5 wanatarajiwa kufika viwanjani kwa ajili ya michuano 51 itakayozishirikisha timu 24.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga