EU yaitoza Facebook faini ya Euro milioni 110
18 Mei 2017Matangazo
Kamisheni hiyo imeituhumu Facebook kutoa taarifa potofu, ikikanusha uwezekano wa kuunganishwa kielektroniki kwa kurasa za mtumiaji za Whatsap na Facebook, ingawa mtandao huo ulifahamu kuwa uwezekano huo upo. Kamisheni ya Ulaya imesema kuwa faini hiyo inahusu taarifa hiyo ya kupotosha, lakini haiondoi ridhaa yake kwa Facebook kuinuua Whatsapp.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya ahusikaye na sera ya ushindani Margrethe Vestager amesema uamuzi wa leo ni ujumbe kwa makampuni mengine kwamba yanapaswa kuheshimu kanuni za kibiashara za umoja huo, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kutoa taarifa sahihi.
Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Bruce Amani