EU kuiunga mkono Ukraine lakini kutoziba pengo la Marekani
6 Oktoba 2023Matangazo
Hofu hiyo imechochewa na mzozo wa kisiasa mjini Washington, uliopelekea Rais Joe Biden kukiri ya kuwa hali hiyo "inamtia wasiwasi" kwamba msaada wa Marekani kwa Ukraine huenda ukayumba. Umoja wa Ulaya na Marekani hutoa mabilioni ya fedha na msaada wa kijeshi kwa Kyiv.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ana imani bado anaungwa mkono na pande zote nchini Marekani huku akisisitiza umuhimu wa misaada kutoka kwa mataifa ya Magharibi katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi.