EU wafikia makubaliano ya kuipatia fedha zaidi Ukraine
1 Februari 2024Matangazo
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel, ametangaza kwamba makubaliano hayo yamefikiwa ndani ya saa moja baada ya kuwasilishwa mjini Brussels.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamekaribisha makubaliano hayo aliyoyataja kuwa ni uamuzi muhimu.
Soma pia:Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakabiliana na Orban kuhusu msaada wa Ukraine
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban, aliandika kupitia ukurasa wa X kwamba watasimama kwa ajili ya sauti ya watu hata kama wanapokea vitisho kutoka ndani ya Umoja huo.
Orban alizusha pingamizidhidi ya mpango wa kuisadia kifedha Ukraine mnamo mwezi Desemba na kutishia kuzuia kupitishwa kwake.