1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kugharamia zaidi NATO

Jane Nyingi
28 Juni 2017

Mataifa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO pamoja na Canada yametangaza kuongeza kiwango cha fedha inachotumia kwa ulinzi kwa asilimia 4.3 mwaka huu wa 2017.

https://p.dw.com/p/2faIs
Jens Stoltenberg
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Kulbis

Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg amesema lengo hasa ni  kuionyesha Marekani  kwamba yamejitolea kugharamia zaidi.Ongezeko hilo linaonyesha kiwango cha juu kuwahi kutolewa na wanachama hao wa jumuiya ya NATO. Mwaka 2015 mataifa hayo  yalitoa asilimia 1.8, huku mwaka uliopita kiwango cha fedha zinazotengewa ulinzi kikaongezwa kwa asilimia 3.3.Takwimu za kiasi cha fedha kitakachotolewa na kila taifa mwanachama zitatolewa kesho baada ya kuidhinishwa na mabalozi wa jumuiya ya NATO, lakini kwa ujumla  matumizi ya  mwaka huu yatakuwa dola billioni 280 na kuongezeka kwa dolla billioni 46 tangu kupunguzwa kwake,hali iliyoipunguzia uwezo muhimu  bara la ulaya  kwa mfano kuongeza  mafuta ya ndege zake za kivita."Fedha hizo dola billioni 46 za Marekani zitatumika kwa mambo chungu nzima.Zitatumika  katika uwekezaji mpya,matifa zaidi wanachama  yanawekeza zaidi  katika  vifaa vipya,na pia kwa hakika zitatumika katika mazoezi zaidi, mishahara na pensheni amesema Stoltenberg.Kwa mujibu wa Stoltenberg miongoni mwa mataifa 27 wanachama wa NATO ni manne tu, Ugiriki, Uingereza, Poland na Estonia yaliyochangia  kiwango cha fedha yanayohitajika mwaka 2016. Romania itatimiza kiwango hicho mwaka huu  huku Latvia na Lithuania  zikifanya hivyo mwaka ujao wa 2018."Ili kuweka mataifa yetu salama, tunahitaji kuendelea kujitahidi kuongeza  fedha zinazotengewa ulinzi na kugawana mzogo huo  miongoni  mwa mataifa wanachama.Tumeanza kuchukua mkondo sahihi  na hii leo  naweza kutangaza maendeleo makubwa zaidi.

Litauen Militärgroßübung der NATO "Iron Wolf 2017"
Majeshi ya NATOPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Kulbis

Bulgaria na Romania zapinga vikwazo dhidi ya Urusi

Maafisa wa  NATO wamesisitiza kuwa wakati  msimamo mkali wa rais wa Marekani Donald Trump ulifanya kupigwa darubini  matumizi ya  ulinzi,vitendo vya Urusi  kuliyakua jimbo la Ukraine la Crimea mwaka 2014 vilikuwa na  athari zaidi huku mataifa wanachama kwa pamoja yakikubaliana kutopunguza matumizi yao. Kwa upande mwengine, marais wa Bulgaria na Romania  wamesisitiza kuwa hawaipingi Urusi,licha ya mataifa hayo mawili ya mashariki mwa ulaya  kuwa wanachama wa NATO na Umoja wa ulaya. Umoja wa ulaya ulikubaliana kuiongezea vikwazo Urusi kuhusiana na  vitendo vyake  nchini Ukraine .Rais wa Bulgaria Ruemen Radev amesema mawasiliano na Urusi yapaswa kuwekwa wazi,ili kuwepo majadiliano yatakayopunguza  mvutano na  kuepuka hatari zinazoweza kutokea. Bulgaria ni  miongoni mwa wanachama maskini zaidi wa Umoja wa ulaya na inategemea sana gesi kutoka Urusi.   

Mwandishi:Jane Nyingi/AP/AFP
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman